Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania

TIRA Logo
TIRA KATIKA ZIARA YA KIMKAKATI MOROGORO, LENGO NI KUTOA  ELIMU YA BIMA NA KUSAJILI WAKALA WAPYA 
15 Aug, 2024
TIRA KATIKA  ZIARA YA KIMKAKATI MOROGORO, LENGO NI KUTOA  ELIMU YA BIMA NA KUSAJILI WAKALA WAPYA 

Mamlaka ya Usimamizi wa Bima (TIRA) kupitia ofisi yake ya Kanda ya Mashariki leo Agosti 15, 2024 timu ya maafisa mbalimbali wametembelea kiwanda cha kusindika tumbaku cha Dimon Morogoro Tobacco Processors Ltd, lengo kubwa likiwa ni kutoa elimu ya bima na hata kuwasajili kama wakala wa bima. 

Kiwanda hicho kina chama cha SACCOS chenye umiliki wa mtaji wa zaidi ya bilioni tatu za kitanzania na pia kina wanachama tarkibani mia mbili.

Katika kikao kilichofanyika kiwandani hapo, uongozi wa SACCOS hiyo umefurahishwa na ujumbe huo  na hata kutazamia kuomba kusajiliwa kama washauri wa bima (broker), suala ambalo wamesema watalifikisha katika kikao cha mwaka cha wanachama wote kinachotarajiwa kufanyika Septemba, 2024 ili kupata ridhaa ya wanachama hao. 

Ziara hizi ni endelevu katika kuendelea kukuza soko la bima hapa nchini. 

#TIRA KWA SOKO SALAMA LA BIMA