Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania

TIRA Logo
TIRA Kinara: Mshindi wa kwanza Mamlaka Bora: Maonesho ya Tanzanite Manyara Trade Fair 2024  
31 Oct, 2024
TIRA Kinara: Mshindi wa kwanza Mamlaka Bora: Maonesho ya Tanzanite Manyara Trade Fair 2024  

Maonesho ya tatu ya Tanzanite Trade Fair 2024, yamemalizika rasmi Octoba 30 2024 mjini Babati mkoani Manyara. Yalifungwa rasmi na Mkuu wa Wilaya ya Babati Mhe. Emmanuela Mtafikolo Kaganda akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Queen Sendiga ambaye alikuwa na majukumu mengine ya kitaifa. 

Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA), ilishiriki kikamilifu kwa kwa kufanya majukumu mbalimbali yakiwemo kuelimisha majukumu ya Mamlaka, kutoa elimu ya bima na kusikiliza maoni  na kujibu maswali mbalimbali ya wananchi. 

Ueledi, Uwajibaji na kujituma kwa wananchi katika Maonesho hayo kumetoa ushindi kwa Mamlaka kwa kupata cheti cha Mshindi wa kwanza kategori ya  Mamlaka kati ya Mamlaka zilizoshiriki Maonesho hayo ambacho kilitolewa na mkuu wa wilaya hiyo. 

TIRA pia iliibuka mshindi wa pili wa banda lililopambwa vizuri (Best Branding Tent) katika Maonesho hayo ya tatu ya Tanzanite Manyara Trade Fair. 

Maonesho hayo yalianza rasmi Octoba 20 na yaliandaliwa na TIRA kanda ya kati Dodoma chini ya Meneja wake Bw. Frank Fred Shangali, Kanda ya Kati inahudumia mikoa ya Manyara, Dodoma na Iringa. 

TIRA inatumia Maonesho haya kama jukwaa la kutoa elimu na kukutana na wadau mbalimbali ili kuendelea kuelimisha jamii kuhusu bima na hatimaye wananchi kutumia bidhaa hizo za bima ili kujikinga na majanga. Kwa upande wa Mkoa wa Manyara ambao unafanya vizuri zaidi katika sekta ya kilimo wafanyabiashara na wakulima waliaswa zaidi kutumia bima ya kilimo ili kulinda mali na mitaji yao. 

#TIRA KWA SOKO SALAMA LA BIMA ‎