Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania

TIRA Logo
TIRA NA ATI WATOA MSAADA KWA WAATHIRIKA WA MAFURIKO HANANG
12 Dec, 2023
TIRA NA ATI WATOA MSAADA KWA WAATHIRIKA WA MAFURIKO HANANG

Tarehe 10 Desemba 2023, Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania TIRA kwa kushirikiana na Umoja wa Kampuni za Bima Tanzania (ATI) kwa pamoja wametoa msaada wa vitu mbalimbali vikiwemo vyakula na vifaa kwa Waathirika wa Mafuriko yaliotokea tarehe 02 Desemba 2023 katika Wilaya ya Hanang Mkoani Manyara. Akikabidhi Vifaa hivyo Kamishna wa Bima Dkt. Baghayo A. Saqware alieleza namna walivyoguswa na tukio hili na ndio maana alifikia maamuzi ya kuzialika Kampuni za Bima ili wachangie walichonacho waweze kusaidia Waathirika hao.

Miongoni mwa vitu vilivyopelekwa ni pamoja na; Mchele kilo 2400, Maharage kilo 1200, Sukari kilo 100, Ngano kilo 500, Mafuta ya kupikia lita 1080, Maziwa ya Kopo 48, Sahani 208, Vikombe 202, Diaba  8 zinazoingia ndoo nane,  Mabegi ya nguo 5, Unga wa Lishe kilo  22, Chupa za Chai 72, Sabuni za maji dumu 12 , sabuni za miche 400, na sabuni za kunawia mikono chupa 72,Chumvi pakiti 1200.

Akitoa shukrani, Mhe, Mkuu wa Wilaya ya Hanang, Bi. Janneth Mayanja alisema kuwa msaada uliotolewa na  Sekta ya bima umegusa Waathirika kwa kiasi kikubwa sana hasa kwa kuzingatia mahitaji ya watoto wadogo kwa kuwapatia maziwa na unga wa lishe. Aliendelea kwa kuhamasisha Taasisi nyingine na Watu binafsi kuiga mfano wa Mamlaka ya Usimamizi wa bima na Kampuni za bima kuja kujitolea kwa chochote watakachojaaliwa.

TIRA- kwa Soko Salama la Bima.