TIRA YASHIRIKI KATIKA KONGAMANO LA KUTOA ELIMU YA USALAMA BARABARANI
28 Aug, 2024
Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) imeshiriki katika Kongamano la kutoa elimu ya Usalama Barabarani ambapo Meneja wa Kanda ya Kati TIRA, Bw. Frank Shangali akimuwakilisha Kamishna wa Bima Tanzania, Dkt. Baghayo Saqware alipata fursa ya kuelezea jinsi Sekta ya Bima kupitia Mamlaka inavyochangia katika kutekeleza sera ya Usalama Barabarani.
Aidha, Sekta ya Bima ikiwa moja ya wadau wanaoshiriki katika Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani mwaka huu, imeendelea kuwahamasisha watanzania wote kuchukua tahadhari kwa kujikinga na kulinda mali zao kwa kukata bima ya vyombo vya moto.
Usalama barabarani ni jukumu letu sote, na bima ndio hatua ya kwanza ya kijikinga.
#TIRA KWA SOKO SALAMA LA BIMA