TIRA YATOA MISAADA HOSPITALI YA SOMANDA NA SHULE YA SEKONDARI BARIADI
28 Aug, 2024
Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) kupitia Kanda ya Ziwa na kwa kushirikiana na kampuni za bima tarehe 23 Agosti, 2024 walitoa misaada mbalimbali katika Hospitali ya Somanda na shule ya Sekondari ya Bariadi, wilayani Bariadi, Simiyu.
Vifaa mbalimbali kwa ajili ya matumizi ya binadamu vilitolewa kama sabuni, taulo za kike, mipira, daftari n.k, pia Mkurugenzi wa wilaya ya Bariadi Ndg. Adrian Jungu alikuwepo katika tukio hilo, akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Kenan Kihongosi.
Baada ya utolewaji wa misaada hiyo, baadhi ya washiriki walipata nafasi ya kufanya kikao mkakati kuimarisha soko la Bima nchini.
Kanda ya Ziwa inahudumu mikoa ya Mwanza, Simiyu, Mara, Geita na Kagera.
#TIRA KWA SOKO SALAMA LA BIMA