TIRA SASA KUWAFIKIA WANA - KATAVI, TIRA TUPO ULIPO
Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) imeendelea na mkakati wake wa kuhakikisha huduma za bima zinawafikia watanzania wengi zaidi.
Katika kutekeleza hilo, Menejimenti ya Mamlaka ikiongozwa na Kamishna wa Bima Tanzania, Dkt. Baghayo Saqware na Naibu Kamishna wa Bima Tanzania, Bi. Khadija Said wamefanya ziara Mkoani Katavi kwenye Ofisi ya Kanda ya Ziwa Tanganyika.
Viongozi hao wameambatana na wajumbe wengine kutoka TIRA wakiwemo Meneja wa Kanda ya Ziwa Tanganyika, Bw. Kurenje Mbura, Meneja Mipango, Bw. Said Mpombo, Katibu wa Kamati ya Ujenzi, Bi. Sophia Mbiku, Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Sheria, Bi. Deodatha Nyika, Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Fedha, Bi. Stella Gama, Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Utawala, Bw. Henry Bayona, Bw. Abubakar Kafumba Afisa Uhusiano Mwandamizi na Afisa Bima, Bw. Maneno Mung’ong’o kwa lengo la kutathmini eneo ambapo kutajengwa rasmi ofisi ya makao makuu ya TIRA Kanda ya Ziwa Tanganyika.
Aidha, Ujumbe huo wa TIRA ulifanya mazungumzo na Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mhe. Mwanamvua Hoza Mrindoko na baadaye Mkurugenzi wa Manispaa ya Mpanda Bi. Sophia Kumbuli kwa ajili ya utambulisho rasmi wa TIRA kwenye Kanda hiyo.
Wakati wa utambulisho huo Dkt. Baghayo Saqware pia alipata fursa ya kuelezea majukumu ya Mamlaka na hatua mbalimbali zilizofikiwa na Sekta ya Bima.
Dkt. Saqware aliendelea kueleza kuwa ili kuwafikia Watanzania wengi zaidi imependekezwa Katavi iwe Makao Makuu ya Kanda ya Ziwa Tanganyika hivyo, ofisi za Kanda zitakazojengwa zitahudumia mikoa ya Katavi, Rukwa na Kigoma.
Aidha, Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe. Mwanamvua Hoza Mrindoko katika kikao hicho ameishukuru na kuipongeza Mamlaka kwa hatua kubwa iliyochukua kuanzisha ofisi ya kanda na makao makuu yake kuwa Katavi.
Ameeleza kuwa sasa bima inasikika zaidi na hiyo indhihirisha kuwa Mamlaka inatekeleza majukumu yake ipasavyo. “Kupitia bandari yetu ya Karema ya Ziwa Tanganyika, na mwingiliano mkubwa kati ya wafanyabiashara wa Tanzania na Congo, ni vyema na wao wakapata elimu itakayowasaidia kulinda mali zao na biashara wanazofanya na nchi jirani”. Alisema Mhe. Hoza.
#TIRAKwaSokoSalamaLaBima