Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania

TIRA Logo
TIRA: WASHAURI WA BIMA ‘INSURANCE BROKERS’ WAPEWA SOMO KUZINGATIA SHERIA NA MIONGOZO MBALIMBALI 
10 Oct, 2024
TIRA: WASHAURI WA BIMA ‘INSURANCE BROKERS’ WAPEWA SOMO KUZINGATIA SHERIA NA MIONGOZO MBALIMBALI 

Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) leo Octoba 1, 2024 imefanya mafunzo kwa madalali/washauri wa Bima kutoka TIBA (Tanzania Insurance Brokers Association). Mafunzo hayo yamefanyika jijini Dar es Salaam yakiwa na lengo la kufundisha na kukumbusha sheria za bima nchini na miongozo mbalimbali kutoka Mamlaka. 

Kwa siku ya pili sasa Kurugenzi ya Sheria kutoka TIRA imetoa mafunzo hayo, ambapo hapo jana Septemba 30, ilitoa darasa kwa Mawakala wa Bima nchini. 

Bw. Okoka Mvigalenzi ni Meneja wa Utekelezaji Sheria na Kushughulikia Malalamiko na alikumbusha na kufundisha kuhusu taratibu mbalimbali zinazotakiwa kufuatwa na Washauri hao zikiwemo ; Kufanya usajili kwa wakati na kutokuuza bima bila usajili ambapo kosa hilo adhabu yake ni faini ya Tsh, milioni tano au kifungo cha miaka miwili au vyote kwa pamoja ikiwa inategemea na usugu wa kosa.

Kuhusu suala la uhuishaji alikumbusha washiriki hao kulipa Ada  kwa wakati, pia makusanyo ya bima ‘premium’ ya yapelekwe kwa wakati na waajiriwa wawe na sifa zinazostahili. 

Bw. Okoka pia aliwatahadharisha juu ya masuala ya Utakatishaji fedha (Money Laundering) katika soko na kuwaasa kuwa makini na mihamala mbalimbali wanayoitilia shaka kujikinga na mkono wa sheria na kuharibu biashara, Pia alikumbusha umakini zaidi kwa waajiri ili kuepukana na kuwaajiri wahalifu au magaidi. 

Nae Raisi wa TIBA Bw. Okoth Oloo aliishukuru Mamlaka kwa mafunzo hayo yanayoongeza maarifa na umakini hasa katika eneo la sheria akisisitiza  kuwa endelevu.Washiriki pia walipewa elimu ya mifumo na kisha kupata nafasi ya kutoa maoni na kuuliza maswali mbalimbali yaliyojibiwa kikamilifu na maafisa wa Mamlaka. Na maoni mengine kuchukuliwa kwa ajili ya kufanyiwa kazi. 

#TIRA KWA SOKO SALAMA LA BIMA