Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania

TIRA Logo
TIRA YAENDELEA KUTOA ELIMU YA BIMA KATIKA MAONESHO YA NANE NANE DODOMA
05 Aug, 2024
TIRA YAENDELEA KUTOA ELIMU YA BIMA KATIKA MAONESHO YA NANE NANE DODOMA

Mamlaka ya Usimamizi wa Bima (TIRA) kwa takribani siku tano mfululizo imeendelea kutoa elimu ya Bima katika Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo, Nane Nane jijini Dodoma. 

Lengo likiwa kuwafikia wananchi wengi zaidi na kutoa uelewa kuhusu bima na hatimaye wananchi hao kunufaika na huduma za bima. Ukifika katika banda letu pia utapata nafasi ya kuwaona wadau wetu ambao ni watoa huduma za Bima na watakuhudumia vizuri.

Kwa kuzingatia dhima ya maonesho haya TIRA tunasema Kilimo na Bima, Bima na Kilimo!. Wadau mbalimbali wa kilimo wanapata nafasi ya kufahamu kampuni zinazokata bima  ya kilimo na pia faida zake ikiwemo kuwalinda wakulima dhidi ya athari za kifedha pale ambapo wanapata majanga mbalimbali ikiwemo kukosekana kwa mvua na ukame.

Lakini sio bima ya kilimo tu, Wananchi pia wanapata nafasi ya kujifunza kuhusu bima nyingine zikiwemo bima za vyombo vya moto, bima za nyumba, bima za maisha, bima za baharini, bima za wakandarasi, bima za mashine nakadhalika.

Njoo tuongee kuhusu Bima, Bima Kinga yako dhidi ya Majanga. Katika viwanja hivi vya Nane Nane jijini Dodoma tunapatikana banda la Private Sector Pavilion number 3. Karibu tukuhudumie.

#TIRA KWA SOKO SALAMA LA BIMA