TIRA YAKUTANA NA MKUU WA MKOA DAR ES SALAAM: KUJADILI NAMNA BORA KUWAFIKIA WANANCHI WENGI UTOAJI ELIMU YA BIMA
Mamlamka ya Usimamizi wa Bima Tanzania -TIRA , ikiongozwa na Kamishna wa Bima Dkt.Baghayo Saqware na Naibu Kamishna Bi Khadija Said leo Agosti 22, 2024 wamekutana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Albert Chalamila Ofisini kwake Ilala Boma na kufanya mazungumzo kuhusu maswala ya bima.
Katika mazungumzo hayo Kamishna wa Bima ametoa rai kwa wananchi kukata bima hasa Bima ya afya kwa wote ili wawe na uhakika wa matibabu lakini pia bima za kukinga mali zao pindi majanga yanapotokea.
Pia ameomba uongozi wa mkoa kuishirikisha TIRA kwenye majukwaa mbalimbali yakiwemo ya wafanyabiashara pamoja na Viongozi wa vitongoji ili kuweza kutoa ellimu ya Bima iwafikie wananchi wengi kwa pamoja.Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Albert Chalamila katika majadiliano hayo ameitaka mamlaka kuendelea kuhamasisha na kutoa elimu ya Bima katika makundi mbalimbali ikiwemo wafanyabiashara wakubwa na wadogo pia watumishi wa umma na binafsi kutambua umuhimu wa Bima.
“Tafuteni namna ya kuielezea bima kwa maneno na mifano hai ili wanachi waweze kuelewa, wakielewa ni rahisi kujenga utamaduni”
Aliongeza Mhe. Chalamila