TIRA YASHIRIKI SIKU YA INDIA SABASABA 2024: BIMA IWE KINGA KWA WAWEKEZAJI
Mamlaka ua Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) imeshiriki hafla ya Siku ya India (Indian Day) kwenye maonesho ya 48 ya Biashara ya Sabasaba 2024 tarehe 11 Julai 2024.
Hafla hiyo fupi inayotarajiwa kuchochea uwekezaji kati ya Tanzania na India imehudhuriwa na wageni mbalimbali wanaoiwakilisha Tanzania na India kutoka katika sekta mbalimbali.
Kupitia halfa hiyo fupi Kamishna wa Bima, Dkt. Bhasghayo Saqware amepata fursa ya kueleza kuhusu Sekta ya Bima kwa na jitihada za TIRA katika kuhakikisha huduma za bima zinabaki kuwa na manufaa na endelevu.
Dkt. Saqware ameeleza kuwa bima ni moja ya sekta zinazokua kwa kasi nchini kwa wastani wa asilimia 15 kila mwaka kutokana na kasi ya uwekezaji unaofanyika hapa nchini. “Uwekezaji unaofanyika nchini ni fursa nzuri ya maendeleo ya uchumi hivyo ni vema kila uwekezaji unaofanyika upewe kinga ya Bima” Alisema Dkt. Saqware