Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania

TIRA Logo
TUNAKUSIKILIZA, KAMISHNA WA BIMA APOKEA MAONI YA WADAU WA KANDA YA ZIWA KUHUSU SEKTA YA BIMA NCHINI
31 Jul, 2024
TUNAKUSIKILIZA, KAMISHNA WA BIMA APOKEA MAONI YA WADAU WA KANDA YA ZIWA KUHUSU SEKTA YA BIMA NCHINI

17 April 2024 Kamishna wa bima Dkt. Baghayo Saqware, amefungua Mkutano wa Kutoa elimu ya bima na kupokea maoni kutoka kwa wadau wa bima walioko Kanda ya Ziwa jijini Mwanza.

Mkutano huo ni wa 3 kufanyika katika kipindi cha miaka 3 mfululizo ambapo mkutano wa kwanza ulifanyika mwaka 2021, wa pili ulifanyika mwaka 2022 na wa 3 ni huu uliofanyika mwaka huu 2024.

Wakati wa kutoa hotuba yake ya Utambulisho Ndg. Richard Toyota, Meneja wa Kanda ya Ziwa aliwashukuru Wadau wote wakiwemo watoa huduma za bima kwa mchango wao mkubwa wanaotoa katika sekta ya bima.

Nae Kamishna wa Bima Tanzania wakati wa hotuba yake alieleza kuwa, TIRA inatekeleza jukumu la kutoa elimu ya bima kwa Umma. Lakini pia inafuata falsafa ya Mabadiliko ya “R” 4 ya Mhe. Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambayo ni Upatanishi au Maridhiano, (Reconciliation) Ustahimilivu (Resilience) Kujenga (Rebuilding) Mabadiliko (Reform).

Falsafa hii inakwenda sambamba na malengo ya sekta ya Bima kwani hata TIRA inaamini kwenye mabadiliko. Katika mkutano huo, Mada mbalimbali ziliwasilishwa ikiwemo Mada ya Bima za vyombo vya moto, Bima za maisha, Bima za Kilimo na Mifugo, Utaratibu wa Fidia na Malalamiko ya Bima, Utaratibu wa kuwa Wakala wa Bima na mada kuhusu Mfumo ya tehama mwisho ilikuwa ni Marekebisho ya Sheria ya Bima. TIRA kwa soko salama la bima.