Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania

TIRA Logo
Utoaji elimu ya bima kwa umma: TIRA yashiriki  Maadhimisho Wiki ya Sheria 2025
25 Jan, 2025
Utoaji elimu ya bima kwa umma: TIRA yashiriki  Maadhimisho Wiki ya Sheria 2025

Utoaji elimu ya bima kwa umma: TIRA yashiriki  Maadhimisho Wiki ya Sheria 2025

Maadhimisho ya Wiki ya Sheria yamefunguliwa rasmi leo Januari 25, 2025 katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam na yanatarajiwa kumalizika Januari 31 2025. Mhe. Sixtus Mapunda, mkuu wa wilaya ya Temeke,akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam amefungua rasmi maadhimisho hayo, yakiwa na lengo la kukutanisha taasisi mbalimbali kutoa elimu na huduma hasa zinazohusu sheria.

Mamlaka ya Usimamizi wa Bima (TIRA) inashiriki maadhimisho haya kwa lengo la kufikisha elimu ya bima kwa jamii , kutoa ufafanuzi wa sheria za bima na kusikiliza changamoto za kibima kutoka kwa wananchi. Ambapo maafisa mbalimbali kutoka Mamlaka wapo kutoa elimu. Maadhimisho hayo yamebeba kauli mbiu ya “Tanzania ya 2050, nafasi yaTaasisi zinazosimamia haki madai katika kufikia malengo makuu ya Dira ya Taifa ya Maendeleo”.

Meneja wa Sheria na Kushughulikia Malalamiko Bw. Okoka Mgavilenzi alitoa elimu ya bima kwa Mkuu wa Wilaya na wadau walioshiriki ambapo alieleza kuhusu uanzishwaji wa Mamlaka, majukumu yake na kuhusu sheria mbalimbali zinazosimamia soko la bima nchini zikiwemo Sheria za Bima ya Afya kwa Wote Na. 13, ya mwaka 2023, ambapo Mamlaka imepewa jukumu la usimamizi na Mhe Mapunda alitoa rai kwa Mamlaka kuendelea kufanya kazi kwa ueledi na uwajibikaji akisisitiza yeye pia ni mnufaika wa kulipwa madai ya kibima. 

Wananchi wote wa jiji la Dar es Salaam na maeneo ya jirani mnakaribishwa sana katika viwanja hivi ili kuweza kupata elimu ya bima na kujibiwa maswali mbalimbali kuhusu changamoto za kibima. 

#TIRA KWA SOKO SALAMA LA BIMA