Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania

TIRA Logo
WAENDESHA PIKIPIKI WAPEWA ELIMU YA BIMA NA KUFUNDISHWA JINSI YA KUTUMIA MIFUMO YA TIRA KUHAKIKI BIMA ZAO
03 Sep, 2024
WAENDESHA PIKIPIKI WAPEWA ELIMU YA BIMA NA KUFUNDISHWA JINSI YA KUTUMIA MIFUMO YA TIRA KUHAKIKI BIMA ZAO

Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) imeendelea na utoaji wa elimu ya bima kwa jamii katika makundi mbalimbali ili kuhakikisha wanawafikia watanzania wengi zaidi ili wajue na watambue huduma za bima. 

Tarehe 31 Aug 2024,  katika viwanja vya Tip top jijini Dar es Salaam, Mamlaka kupitia ofisi yake  ya Kanda ya Mashariki  inayodumu mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro,na Pwani kwa kushirikiana na wadau wa bima, imetoa elimu ya bima katika Bonanza la Bodaboda  ambapo waendesha bodaboda walipata fursa ya  kufahamu mfumo wa kuhakiki chombo cha moto kupitia TIRA-MIS.

Aidha waendesha bodaboda hao walielezwa umuhimu wa kukata bima na gharama za bima kwa usafiri wa bodaboda, zaidi ya hapo, walipata fursa ya kuuliza maswali yaliyopatiwa majibu papo hapo.Ujumbe wa TIRA uliongozwa na Afisa Bima Ndg Mfoi pamoja na Haiba,Abdul, Islam, John na  Kalebi Chiya.

#TIRA KWA SOKO SALAMA LA BIMA