Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania

TIRA Logo
Wajumbe Baraza la Wafanyakazi TIRA wanolewa wajibu na majukumu yao, Bw. Joseph Oguda aibuka mshindi Katibu wa Baraza
03 Dec, 2024
Wajumbe Baraza la Wafanyakazi TIRA wanolewa wajibu na majukumu yao, Bw. Joseph Oguda aibuka mshindi Katibu wa Baraza

Wajumbe Baraza la Wafanyakazi TIRA wanolewa wajibu na majukumu yao, Bw. Joseph Oguda aibuka mshindi Katibu wa Baraza

Mafunzo ya Baraza la nne (4) la watumishi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania yanafanyika leo katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa mjini Babati mkoani Manyara. Mada mbalimbali zitafundishwa kwa wajumbe lakini pia uchaguzi wa katibu na katibu msaidizi umefanyika. Disemba nne (4) na tano (5),2024 utafanyika Mkutano wa Kwanza wa Baraza la Wafanyakazi 2024.

Naibu Kamishna wa Bima Tanzania Bi. Khadija Said akifungua mafunzo hayo amewataka watumishi wa Mamlaka kuendeleza utii, uadilifu na kujitoa katika kazi mbalimbali, pia kuwataka viongozi wa Baraza hilo waliochaguliwa kufanya kazi kwa weledi na uadilifu.   

Bw. Joseph Oguda na Bi. Nasra Dodo kutoka Mamlaka waliwania nafasi ya Katibu  wa Baraza hilo ambapo Bw. Oguda alishinda nafasi hiyo wakati Bi. Nasra atahudumu kama Katibu Msaidizi.

Mada zinazowasilishwa ni pamoja na Wajibu na Majukumu ya mjumbe wa Baraza, Umuhimu wa TUGHE mahali pa kazi na Wasilisho kutoka mfuko wa Hifadhi ya Jamii (PSSSF). 

Nini Umuhimu wa Baraza la wafanyakazi ?,  Baraza huwaleta pamoja watumishi katika ushirikishwaji na taasisi , pia ni chombo cha mawasiliano katika idara, vitengo na ofisi za kanda na ngazi ya menejimenti ambapo hutoa maoni na changamoto mbalimbali kuhusu kazi zao. Lakini pia Baraza husaidia kupunguza na kuondoa migogoro sehemu za kazi. 

#TIRA KWA SOKO SALAMA LA BIMA