Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania

TIRA Logo
WATUMISHI WA SERIKALI WILAYA YA BAHI WAPEWA DARASA LA BIMA
10 Oct, 2024
WATUMISHI WA SERIKALI WILAYA YA BAHI WAPEWA DARASA LA BIMA

Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) ina jukumu la kutoa elimu ya bima kwa wananchi, ili waweze kuelewa umuhimu wake na kutumia bidhaa mbalimbali za bima ambazo ni ulinzi na kinga wakati wa majanga.

Kupitia ofisi zake za Kanda zilizopo nchi nzima TIRA inatoa elimu kwa njia mbalimbali zikiwemo mikutano, semina kwa wadau mbalimbali.

Octoba 7, 2024 Katika mafunzo maalumu yanayohusu Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wilayani Bahi, Mamlaka kupitia Kanda ya Kati ilipata nafasi ya kutoa elimu ya bima kwa watumishi wa serikali wiłayani hapo wapatao 421 wakiwemo walimu na watendaji kata na vijiji ambao walipata somo kuhusu bima za moto, bima ya nyumba, bima za vyombo vya moto, bima ya afya, bima ya kilimo na nyinginezo.

Wananchi hao pia walipewa elimu ya Bima ya Afya kwa Wote yenye lengo la kuhakikisha kila mtu anapata huduma ya afya kulingana na kipato chake, pia walifundishwa kuhusu mifumo ya uhakiki bima na hatua za kufuata katika kufatilia madai mbalimbali ya bima.

Meneja wa Kanda hiyo Bw. Frank Shangali alishukuru uongozi wa Halmashauri ya Bahi kwa nafasi waliyotoa kwa Mamlaka ambapo kupitia mafunzo hayo wahusika watakuwa mabalozi wazuri wa bima na kutoa elimu zaidi kwa watu wengine na hata kuanza kutumia huduma hizo.

#TIRA KWA SOKO SALAMA LA BIMA