Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania

TIRA Logo
Elimu ya TAKAFUL yatolewa kwa wanafunzi wa MUM
12 Apr, 2025
Elimu ya TAKAFUL yatolewa kwa wanafunzi wa MUM

Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) imetoa elimu ya Takaful kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha  Kiislam Morogoro (MUM) ikiwa ni utekelezaji wa mikakati mbalimbali ya kutoa elimu ya bima kwa umma kupitia makundi tofauti ya jamii, vyombo vya habari, mitandao ya kijamii n.k. 

Elimu ya Takaful kwa wanafunzi hao imetolewa mapema tarehe 10 Aprili 2025 katika ofisi ya TIRA iliyopo Mtendeni na wataalam wabobezi ambao ni Bw. Paul Ngangaji na Bi. Raya Abdallah (Maafisa bima) ambao walieleza sekta ya bima nchini imekata kiu ya Watanzania wengi ambao walikuwa hawakati bima kutokana na sababu mbali mbali ikiwemo imani ya kutotaka Riba.
Takaful ni mfumo wa bima wa ushirikiano unaozingatia misingi ya Shariah, ambapo wanachama huchangia fedha kwa pamoja ili kusaidiana katika kukabiliana na hasara au majanga yanayoweza kutokea

Akitoa shukrani zake za dhati mwalimu aliyeambatana na msafara huo aliishukuru Mamlaka alisema kuwa wanafunzi hao wamepata kitu chema na ambacho hakitatoka kwenye vicha vyao

TIRA kwa soko salama la bima.