TIRA: Tunaboresha Usalama vyombo vya moto tupo bega kwa bega na Jeshi la Polisi kuongeza ufanisi

Aprili 28, 2025 TIRA kupitia Kanda ya Mashariki imekutana na jeshi la polisi kuzungumzia uboreshaji usalama barabarani na ufanisi wa matumizi ya bima, maongezi hayo yamefanyika katika maonesho ya Kazi za Utamaduni na sanaa yanaendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja hapa jijini Dar es Salaam ambapo Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) inashiriki kama sehemu ya kuwahamasisha wasanii kukata bima na kuunga mkono kazi za sanaa kwa kutoa elimu ya bima kwa wananchi mbalimbali wanaotembelea maonesho hayo.
Meneja wa TIRA Kanda ya Mashariki Bw. Zakaria Muyengi ameelezea kazi za kanda hiyo inayohudumu mikoa ya Dar es Salaam, Pwani na Morogoro wakati wa ugeni wa Jeshi la polisi uliotembelea banda la TIRA ambao uliongozwa na Mkaguzi Msaidizi Masjala ya Polisi Afande RPS Bi. Rose Tittey wa Mkoa wa Kipolisi wa Ilala.
Aidha katika mazungumzo yao, wamekubaliana na kupanga kuboresha mahusiano kati ya TIRA na mkoa wa kipolisi Ilala katika shughuli mbalimbali zinazohusiana na bima hasa uhalifu kwenye bima za vyombo vya moto, elimu ya bima kwa jeshi la polisi na kushirikishana fursa zilizopo katika soko la bima kama saccos ya jeshi la polisi kufanya shughuli za uwakala wa bima.
Jeshi la polisi Tanzania ni moja kati ya wadau wakubwa wa Mamlaka kwa sababu ya ushirikiano uliopo katika kazi za ufatiliaji hasa wa bima za vyombo vya moto kama gari na pikipiki.
TIRA imeendelea kutoa wito kwa Wananchi kutembelea banda la Mamlaka ili kupata elimu ya bima katika maonesho hayo ambayo yalianza rasmi tarehe 24 Aprili na kutarajiwa kumalizika rasmi tarehe 30 Aprili 2025.
TIRA KWA SOKO SALAMA LA BIM