Wanawake TIRA washiriki mkutano TAWiFA, fursa sekta ya Bima zaelezwa

Wanawake TIRA wamejumuika na Wanawake wengine kutoka sekta ya Fedha Tanzania Aprili 16 2025 Dodoma kushiriki Mkutano Mkuu wa Mwaka ulioandaliwa na jumuiya yao (TAWiFA) ambapo DKt. Doto Biteko alikua Mgeni Rasmi.
Akisoma hotuba yake Mhe. Biteko alisisitiza juu ya elimu ya fedha kwa wanawake wa vijijini ili waepukane na mikopo umiza inayosababisha kuchukuliwa baadhi ya mali zao za ndani wanaposhindwa kurejesha mikopo hi
Kwa upande wake Naibu Kamishna wa Bima Bi. Khadija Issa Said ameeleza namna sekta ya bima ilivyokua nchini huku wanawake katika sekta hiyo wakitoa mchango mkubwa kupitia uongozi makini lakini ufanyaji kazi wao katika nafasi mbalimbali.
Bi. Khadija aliwataka wanawake kwenye sekta ya fedha kuendelea kujibiidisha kazini na kushirikiana ili waendelee kukuza sekta ya fedha.
Aidha Bi. Fikira Mtomola, Rais wa TAWiFA alisema mkutano huo wenye kauli mbiu ya “Wekeza kwa wanawake ili kuchochea maendeleo” una lengo la kuongeza uelewa na uwajibikaji wa wanawake katika sekta ya fedha nchini na kutengeneza mazingira wezeshi kwa wanawake ili kujumuishwa na kuongoza katika mambo mbalimbali ya kifedha.
Mkutano Mkuu huo uliofanyika Aprili 14, 2025 Jijini Dodoma ulihudhuriwa pia na Viongozi mbalimbali akiwemo Dkt. Angela Kairuki Mshauri wa Rais na Waziri wa Maliasili na Utalii, Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Mgeni Hassan Juma, Naibu Waziri wa Fedha, Bwn. Hamadi Chande na wengine wengi.
Mkutano huo ulitanguliwa na matukio mbalimbali ambapo tarehe 11 Aprili 2025 kulikua na upandaji wa Miti ya Matunda zaidi ya 2000 katika Shule za Msingi za Mkoa huo, tarehe 12 Aprili 2025 utoaji elimu ya fedha kwa wanawake wajasiriamali iliyofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Zabibu, Dodoma.